Header Ads

Header ADS

Wabunge wa CHADEMA waliohojiwa na TAKUKURU wafikia 42




Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Wabunge wa chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, wameendelea kuhojiwa na taasisi ya kuzuia ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Makao Makuu Dodoma juu ya matumizi mabaya ya fedha za michango ya wabunge wa chama hicho.

Mwendelezo wa mahojiano hayo yanafanya kufikia idadi ya wabunge wa chama hicho waliohojiwa kufikia 43 ambapo lengo la Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa imetaka kujua matumizi ya fedha ambazo zimekuwa zikichangwa na wabunge hao.

Hivi karibuni baadhi wabunge wa CHADEMA kwa wakati tofauti walitangaza kukihama chama hicho kwa madai ya kuchangishwa fedha lakini tutojua namna fedha hizo zinavyotumika huku wengine wakidai kunyanyaswa kingono.

Baadhi ya wabunge waliohojiwa siku ya leo ni Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema, Mbunge wa Tarime vijijini John Heche, Sophia Mwakagenda, Cesilia Pareso, Mariam Msabaha.

Wengine ni Joyce Sokombi, Susan Masele, Anna Gidalia, Zainabu Bakari, Conchesta Lwamlaza, Grace Tendega, Sabrina Sungura, Lucy Mageleli, Lucy Owenya, Joseph Makumbi.

Zoezi la kuwahoji wabunge hao litaendelea siku ya jumatatu ili kutimia kwa wabunge sitini na tisa wanaotarajiwa kuhojiwa na taasisi hiyo.



No comments

Powered by Blogger.