Tanga ya Pili kwa Madawa ya Kulevya
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuboresha huduma za afya nchini ambapo Tsh. Milioni 780 zimetolewa kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma za methadone kwa waathirika wa dawa za kulevya katika mkoa Tanga wenye watumiaji 5190 wa dawa hizo kwa takwimu za mwaka 2016.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa dawa za kulevya kilichopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga - Bombo.
“Leo nina amani moyoni, ilikuwa ndoto yetu, tumepambana sana kuhakikisha tunaleta huduma za methadone kwa waathirika wa madawa ya kulevya, Tanga inashika nafasi ya pili kuwa na watu wengi wanaotumia dawa za kulevya,” -UMMY
No comments