Shilole: Wolper Anapenda Mwanaume Wenye Hela
BAADA ya msanii wa filamu, Jackline Wolper, kuvishwa pete ya uchumba hivi karibuni, msanii wa muziki na filamu, Zuwena Mohamed, amefunguka kuwa msanii huyo anapenda mwanaume mwenye hela.
Shilole amesema kuwa ni jambo la heri Jackline kuvishwa pete, japo kwa upande wake anapenda sana hela hivyo mwanaume wa kumuoa lazima awe na hela.
“Mimi na Jackline tuna ukaribu sana, ni mshikaji wangu, ni jambo la heri yeye kuvikwa pete, japo anapenda sana hela, najua hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hana hela,’’ alisema Shilole.
Stori: Happyness Masunga
No comments