RPC Arusha Ahamishwa Kituo cha Kazi
Viongozi wa mkoa wa Arusha waliosamehewa na Rais Magufuli, wamehamishwa vituo vyao vya kufanyia kazi ikielezwa kuwa ni hatua ya kuboresha ufanisi wa kazi ndani ya mkoa huo.
Kamanda Jonathan Shana ambaye alikuwa RPC wa Arusha amehamishiwa katika chuo cha polisi CCP mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa TAKUKURU Frida Wikes amehamishiwa katika ofisi za mako makuu.
Imeelezwa kuwa kiongozi mwingine aliyeathirika na uhamisho ni mkuu wa usalama wa mkoa huo.
Ikumbukwe kuwa juzi jumatatu, Rais Magufuli alitangaza kuwasamehe viongozi hao na kuwapa onyo la mwisho kwa kosa la kufanya kazi ambazo hajawatuma yeye.
No comments