Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli Arejesha Fomu za Kugombea Urais Kupitia CCM....Wanachama Zaidi ya Milioni 1 wa CCM wamdhamini



Jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 wa  chama cha Mapinduzi, CCM wamejitokeza kumdhamini Mwenyekiti wao Rais Magufuli katika fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally wakati wa hafla fupi ya  kuzipokea Fomu za Kugombea Urais wa Tanzania Zilizowasilishwa na Rais Magufuli

Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama Milioni 1,023, 911 walijitokeza kumdhamini  Rais Magufuli kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.

Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.

No comments

Powered by Blogger.