Petit Man Akubali Yaishe Kwa Esma!
Mapenzi yanauma jamani! Kama huamini sikiliza kilichompata meneja wa wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, Hamad Manungwi ‘Petit Man’ baada ya aliyekuwa mkewe, Esma Khan kuvishwa pete ya uchumba.
Mapema wiki hii, Esma ambaye ni dada wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alivishwa pete ya uchumba na mfanyabishara mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Tesha.
Akifunguka mbele ya Gazeti la IJUMAA baada ya mzazi mwenzake huyo kuchumbiwa, Petit Man Wakuache ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na Esma aitwaye Taraj alisema alijua muda mrefu kwamba mwenzake huyo alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine.
“Unajua watu wanashindwa kuelewa kabisa kuwa mimi na Esma tulishamalizana siku nyingi mno hivyo watu wanaosema kuwa nimejifungia ndani kwa maumivu, siyo kweli, ninaendelea na maisha yangu,” alisema Petit Man akisisitiza kuwa alishakubali yaishe kati yake na Esma.
Aliendelea kusema kuwa, Esma anamheshimu mno kama mama aliyemzalia mtoto wake wa kipekee Taraj na tayari yeye ana uhusiano wake mwingine.
“Kwanza kwa sasa mimi nina maisha yangu mengine kabisa. Ninamuombea heri kwenye maisha yake mapya na mimi ninaendelea na maisha yangu, nitaendelea kushirikiana naye kulea wangu tu na si vinginevyo,” alisema Petit Man.Tangu waoane, Esma na Petit Man wamekuwa wakiachana na kurudiana kwa zaidi ya mara tatu, lakini sasa inaonekana ndiyo jumla baada ya mwanamama huyo kuvishwa pete hiyo ya uchumba.
No comments