Header Ads

Header ADS

Ndoa ya Siri Ya Ben Pol Yatikisa





MAZITO yameibuka baada ya kuvuja siri ya ndoa ya mwanamuziki wa Bongo Fleva Benard Paul ‘Ben Pol’, kufunga ndoa ya siri na mchumba wake wa siku nyingi Anerlisa Muigai ambaye ni raia wa Kenya.


Habari hizo zilianza kusambaa mitandaoni, baada ya mpishi wa Keki ya Harusi hiyo, anaetumia jina la mom- gemin katika mtandao wa Insta na kuandika maneno haya “We were honored to do #Anna and # benpol wedding cake yesterday. Thanks a lot Anerlisa”, yalisomeka hivyo.

 

Baada ya muda, mwanamama Anerlisa ambaye ndiye mpenzi wa Ben Pol, akapost Insta Live akiandika “A queen can now sit on her throne comfortably’’, yalisomeka hivyo na kusindikizia picha ya Malkia akiwa amekaa kwenye kiti na taji juu yake.



Hiyo iliwafanya watu waamini ni kweli ndoa imefungwa japo wananzengo walitoa mapovu kama yote kwa mwanamama huyo, kwani ametoka kufiwa na mdogo wake siku za hivi karibuni, kwanini amefanya haraka hivyo.

 

Taarifa ni kwamba, wawili hao waliamua kufanya hivyo NDOA YA…kutokana na janga la virusi vya Corona, hivyo ikawa ni ndoa iliyohudhuriwa na wanafamilia tu.

 

BEN POL ATAFUTWA Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, Ben Pol alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, simu yake ya mkononi haikupatikana.




No comments

Powered by Blogger.