Header Ads

Header ADS

Ndege Yaanguka Mexico, Watu Sita Wapoteza Maisha



Watu sita wamepoteza maisha baada ya kuanguka kwa ndege ndogo katika jimbo la Chihuahua nchini Mexico.

Kulingana na taarifa zilizopatikana,ndege hiyo ndogo, aina ya TU206G, ambayo iliondoka katika mji wa mashariki wa Camargo kwenda Sinaloa, ilianguka katika mkoa wa Chihuahua.

Mamlaka yammetangaza kuwa Leonilo Gonzalez Olivas na watu 5 wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

Uchunguzi rasmi umezinduliwa kuhusiana na ajali hiyo.



No comments

Powered by Blogger.