Header Ads

Header ADS

Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson atangaza kugombea ubunge



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson leo ametangaza nia ya kugombea Ubunge, katika jimbo ambalo hakulitaja na kusema kuwa muda ukifika atatoa taarifa ya wapi ataenda kugombea.

Dkt. Tulia ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma katika mkutano wa 19, kikao cha 46 alipopewa nafasi ya kuzungumza ambapo pamoja na kuweka wazi kusudio la kugombea, pia ameipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ilizochukua kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo.

“Nami nimepata hamasa ya kujitosa. Na Inshallah Mwenyenzi Mungu atujalie uzima na afya, yumkini nitakwenda mahali fulani, kuomba ridhaa ya wananchi wenzangu ya kuwatumikia katika bunge lako [Spika wa Bunge] tukufu,” amesema Tulia.

Aidha, kiongozi huyo hajaweka wazi atagombea jimbo gani, lakini kumekuwapo tetesi kuwa huenda akagombea katika Jimbo la Mbeya Mjini ambalo sasa linaongozwa na Mbunge Joseph Mbilinyi kupitia CHADEMA.

Novemba 2015 baada ya kuingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli alimteua Dkt. Tulia kuwa mbunge ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

No comments

Powered by Blogger.