Mitambo mipya ya vitambulisho kuanza Kazi hivi karibuni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema mitambo mipya ya uzalishaji wa vitambulisho vya taifa ambayo inauwezo wa kuzalisha vitambulisho 180,000 kwa siku, itaanza kufanya kazi hivi karibuni baada ya wataalamu kuwasili nchini.
Mitambo hiyo ya kisasa ambayo inauwezo wa kuzalisha vitambulisho 180,000 kwa siku, ilishafungwa muda mrefu ofisini za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), na ilipaswa iwe imenza kufanya kazi tangu mwezi Aprili, mwaka huu lakini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona ilichelewa kuanza kufanya kazi kutokana na watalaamu wa mitambo hiyo kutoka Ujerumani kushindwa kuja nchini.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya na Ipela, jimboni kwake Kibakwe, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, leo, baada ya kupokelewa kwa shangwe kwa kumpongeza kwa kuchaguliwa kuiongoza Wizara hiyo, Simbachawene amesema Watanzania waondoe shaka kwani kupatikana kwa mitambo hiyo ambayo sasa itafanya kazi muda wowote kuanzia sasa baada ya wataalamu kutoka nchini Ujerumani kuwasha mitambo hiyo.
Aidha, Waziri Simbachawene alisema kutonakana na utendaji kazi wa Rais Dkt. John Magufuli, upinzani umekufa wenyewe nchini hivyo uchaguzi ujao chama tawala kimejingea uwezo mkubwa wa ushindi wa kishindo.
Pia alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejenga na inaendelea kujenga miradi mikubwa ambayo inaifanya Tanzania kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kikao hicho, Emmanuel Kagali, alimpongeza Waziri Simbachawene kwa utendaji wake wa kazi ndani ya Jimbo la Kibakwe, kutokana na uwepo wa umeme katika vijiji vyote, ujenzi wa zanahani na barabara.
Waziri Simbachawene anaendelea na ziara yake jimboni humo kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa chama pamoja na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.
No comments