Header Ads

Header ADS

Mfahamu Mwanaume Anayelisha FISI ili Wasiwashambulie...Wanamwita "Hyena Man"



Abbas Yusuf maarufu kama 'Hyena Man' kutoka Harar, Ethiopia amesema alijifunza kulisha wanyama pori kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa na tabia ya kuwarushia mabaki ili kuwaondoa karibu na mifugo

Yusuf huning'iniza kipande cha nyama hewani na badala ya fisi kumshambulia, husogea mbele na kukichukua mkononi mwake kama mbwa wa nyumbani ambaye amepewa mafunzo

Awali, wanyama hao walikuwa wakishambulia watu na hata kuwaua, lakini wakatafuta suluhu kwa kutengeneza matobo ukutani na kuwarushia chakula ili wasile watu. Inadaiwa kuwa hakuna shambulio na fisi kwa miaka 200 sasa

Tofauti na hali halisi sehemu nyingi duniani, wakazi wa Mji wa Harar nchini Ethiopia wana historia ya kuishi kwa amani na fisi na utamaduni huo wa miaka mingi sasa umegeuka kivutio maarufu cha utalii

No comments

Powered by Blogger.