Mchezaji Djokovic Athibitisha ana Virusi vya Corona
Kinara wa Tennis kwa ubora duniani upande wa wanaume Novak Djokovic pamoja na mkewe Jelena Djokovic wamekutwa na Virusi vya Corona baada ya mwenyewe mchezaji huyo kuthibitisha.
Djokovic, mwenye umri wa miaka 33 raia wa Serbia ni mmoja kati ya wachezaji wanne ambao walishiriki kwenye michuano ya Adria Tour kukutwa na Virusi hivyo.
Adria Tour ni maonyesho ya Tennis ambayo yalifanyika nchini Serbia na Croatia katika wiki mbili zilizopita, yamefanya wachezaji wanne kukutwa na Corona akiwemo Grigor Dimitrov, Borna Coric na Viktor Troicki.
Urais 2020: Mwanamichezo achukua fomu Zanzibar
Hata hivyo mke wa Djokovic naye alikutwa na Virusi hivyo, ambapo wote kwa pamoja watajitenga kwa siku 14 mpaka pale afya zao zitakapokuwa vizuri.
No comments