Mbowe Atema Cheche Asema Hawatafuti Dola kwa Sababu ya Tamaa ya Madaraka
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ametema cheche kuwa hawaendi kwenye uchaguzi kuomba kuwa Chama kikuu cha upinzani wanakwenda kusaka dola.
Mbowe aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi wa Bavicha na Chaso walivyokwenda nyumbani kwake kumjulia hali baada ya kushambuliwa mkoani Dodoma na watu wasiojulikana.
‘Vyama vingine vinakwenda kutafuta wabunge na madiwani chama pekee nchini leo chenye uwezo wa kusema tunakwenda kutafuta serikali ya Jamhuri ya Muungano ni Chadema wengine wanaangaika kupata wabunge sijui watatu, tutatangaza wabunge wawili, madiwani wanne sisi tunatafuta dola,” alisema Mbowe.
“Hatutafuti dola kwa sababu ya tamaa ya madaraka tunatafuta dola kwa sababu ya haki na hasira yetu ni kuibadilisha nchi hii kuwa nchi bora zaidi ya kuishi, kuwa nchi yenye furaha, nchi yenye fursa kwa kila mtu, nchi yenye kuheshimu imani za watu,” alisema
Mbowe alisisitiza kuwa hawaendi kutafuta dola ili wakajenge madaraja na kununua ndege ‘Tunakwenda kuitafuta dola tukalete furaha na maisha bora kwa watu wetu. Watu wetu wakishakuwa na maisha bora, furaha na haki ikiwepo ndani ya taifa, amani ikiwepo ndani ya taifa ndege zitanunuliwa, majengo yatajengwa na treni zitajengwa,”
Alisema lengo lao la msingi haliendi kujenga barabara wakasahau haki za watu, furaha na ustawi.
“Unapokuwa na serikali yenye jeuri ya kwenda miaka mitano bila kuongeza mshahara wa watumishi wa umma wakati gharama za uchumi zinapanda,”alisema Mbowe.
"Hatuendi kwenye uchaguzi kuomba kuwa Chama Kikuu cha Upinzani, tayari sisi ni Chama Kikuu cha Upinzani, tunakwenda kwenye uchaguzi kutafuta Dola." Mhe. @freemanmbowetz pic.twitter.com/tadWn1D2OQ— Official Bavicha Taifa (@bavicha_taifa) June 30, 2020
No comments