Kisa Dini, Awagomea Ali Kiba na Harmonize....
Mrembo wa muziki wa Injili Bongo Pinela, amekuwa akisumbuliwa na wasanii wa BongoFleva kwenye DM za mtandao wa Instagram wakimtaka wamtumie kama video vixen kwenye kazi zao.
Kutoka kushoto ni Alikiba, kati ni msanii wa Injili Pinela na Harmonize
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, msanii huyo wa Injili amesema hata akifuatwa na Alikiba au Harmonize hataweza kufanya kazi zao, pia wapo ambao wanamfuata kwa dau kubwa kabisa kuanzia Milioni 3.
"Wasanii wa kiume wa BongoFleva wameshawahi kunifuata, tena walikuwa wanakuja na dau kubwa sana kuanzia Milioni 3 huko, ila mimi tayari nimeshaokoka itakuwa ngumu kwenda huko kwa hiyo siwezi kufanya kazi za kidunia" amesema Pinela.
Akizungumzia endapo akifuatwa na wasanii kama Harmonize au Alikiba, wakitaka kumtumia kwenye kazi zao mrembo huyo amesema "Hapo pagumu na wote nawapenda ila sitaenda hata kwa mmoja, siwezi kufanya nao kazi kwa sababu mimi ni mtu wa injili wao wanafanya kazi za kidunia".
No comments