Kimenuka..Kampuni ya Moil Yalipa Faini ya Tsh Milioni 10 Kwa Kuhujumu Mafuta
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesitisha kufuta leseni ya Kampuni ya Mansoor Oil Industries Limited (MOIL) baada ya kuomba msamaha na kulipishwa faini ya Tsh. Milioni 10
EWURA imesema kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Olympic Petroleum lipo pale pale baada ya kukaidi maelekezo. Iliamriwa hadi jana saa 11 jioni iwe imesambaza mafuta katika maeneo waliyoelekezwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema kutokana na taarifa za uhaba wa mafuta nchini, wamekuwa wakifuatilia hali ya upatikanaji wake kwa kutumia wakaguzi wake na kupata taarifa kutoka kwa Viongozi wa Wilaya au Mikoa
No comments