Johari "Wasanii wa Sasa Wanakuru"puka
Msanii mkongwe kwenye Tasnia ya Filamu hapa Nchini Johari Chagula ”Johari” amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa sasa hivi hawafanyi kazi kwa uweledi bali wanafanya kazi kwa kurupuka.
Akizungumza na Amani Johari amesema kuwa sanaa ya zamani walikuwa lazima mtu uingie kwenye mafunzo ufundishwe jinsi ya kuigiza lakini ni kwa sasa hivi imekuwa tofauti yani kila mtu amekuwa msanii.
“Kwenye mambo ya uigizaji kuna mambo mengi sana yamebadilika kwa sababu sanaa ya zamani ilikuwa ni sanaa ya mapokezi kwahiyo kile tulichokuwa tukikifanya watu wanakipokea kwa mashamsham kwa sababu kilikuwa na mafuzo ndani yake lakini sanaa ya sasa hivi imebadilika kwa sababu hadi watazamaji nao wanajiona ni wajuaji na pia kuna wasanii ambao wanababaisha kwenye suala zima la uigizaji uigizaji wa sasa watu wanakurupuka tu na kwenda kushuti ila sisi tulikuwa tunaingizwa kwenye mafunzo mpaka ujue ndo uigize,” alisema johari.
Stori: Khadija Bakari
L
No comments