Huyu Hapa Malkia Amanirenas Shujaa wa Kiafrika Aliyeishinda Dola ya Kirumi
Kwa ufupi tu Malkia Candace Amanirenas ama KENDAKE alikuwa malkia wa ethiopia ya kale yaani KUSH EMPIRE ambayo kwa kipindi hicho utawala wa meroe ulikuwa Sudan ya sasa.
Alitawala kuanzia 40 BC mpaka 10 BC. Alijizolea umaarufu mkubwa baada ya kuwa kiongozi imara mwanamke shujaa ambaye aliweza kuitawala dola kubwa bila mfalme hivyo kujijengea heshima kubwa.
Mwanamama huyu alikuwa na jicho moja tu baada ya jingine kuwa limetoboka wakati wa moja ya vita na warumi ila pamoja na hayo bado alikuwa na uwezo mkubwa sana kwenye uwanja wa vita na alipigana kishujaa bila uoga.
UMAARUFU WAKE
Alijizolea umaarufu baada ya kuiongoza KUSH kwenye vita iliyodumu kwa miaka 5 yaani 27-22 BC dhidi ya Roman empire waliokuwa wameitawala dunia ya wakati huo na kwa muda huo walikuwa wameitawala misri.
Baada ya vita kali wazungu hao walipigwa na kufurushwa kutoka misri ya kusini kwa kuteka miji muhimu ya Syrene, Philae, na Elephantina, ila baadae warumi wakajipanga na wakarudi vitani na walipoona vita inawadhoofu mwishoni wakaamua kuheshimu mipaka ya wakush hao na wakasaini mkataba wa amani hivyo ushindi huu uliodhihirisha nguvu ya mtu mweusi kupinga ubeberu na ubabe wa wazungu.
Ni tukio la kishujaa sana na limemzolea mwanamama huyu umaarufu mkubwa ukizingatia Dola ya Rumi ilikuwa ndio yenye nguvu na kuogopeka sana wakati huo ni sawa na Marekani ya sasa.
HITIMISHO
Ingawa historia za namna hii hazifundushwi mashuleni tunaishia kufundishwa tu kuhusu ukoloni na jinsi tulivyopigwa kwenye majimaji resistance!!!
Ni wakati umefika sasa historia za namna hii zitunzwe na kuelezwa ili waafrika tuache kuwa na inferiority complex kwa wazungu na kuaminishwa hakuna tunaloweza wakati miaka ya nyuma tuliwahi kuwa na falme zetu zenye dola kamili inayojiendesha kwa mifumo thabiti bila kuomba misaada kwa wazungu.
No comments