Huu hapa ukweli kuhusu Rapa Tekashi69 kupigwa pini facebook, live IG
Ni headline nyingine hii ni baada ya kuibuliwa kwa mashtaka yanayo muhusu kuwatumia watoto kingono kufufuliwa na kupelekea watu wengi kudai mkali huyo anafaa kuadhibiwa na mitandao kama Facebook na Instagram kumuondolea uhalali wa kuitumia.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, baada ya majadiliano na ufatiliaji wa kina wa hoja hizo, imeelezwa kwamba mitandao hiyo haijamkuta na hatia rapa huyo, hivyo haitochukua hatua zozote dhidi yake.
Imeelezwa kuwa, wakati #Tekashi69 anatekeleza makosa hayo alikuwa na umri mdogo na jina lake halijawahi kuandikwa kwenye kumbukumbu za wakosaji wa kingono.
No comments