Gigy Money "Siwezi Kurudiana na Mo J"
Msanii wa Bongo Fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema kuwa hafikirii kurudiana na mzazi mwenzake Mourad Alpha ‘Mo J’ kama ambavyo watu wengi wanavyodhani.
Akipiga stori na Amani hivi karibuni, Gigy alisema kwamba asilimia kubwa ya mashabiki zake wanatamani arudiane na mzazi mwenzake huyo, jambo ambalo yeye binafsi halifikirii kabisa kwa sababu kila mtu kwa sasa ana maisha yake.
“Unajua mimi siishi kwa ajili ya kuwafurahisha watu, naishi vile roho yangu inapenda, siwezi kuwafurahisha watu halafu mimi ndani naumia, najua watu wengi waliipenda kapo yangu na mzazi mwenzangu, lakini haiwezi kuwa kama zamani tena kwa sababu kila mtu ana maisha yake kwa sasa,” alisema.
Stori: Memorise Richard
No comments