Dogo Janja Afunguka Madee Kumnunulia Gari
MSANII wa tasnia ya Bongo Fleva, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’, amekanusha taarifa za kununuliwa gari na msanii mwenzake Hamadi Ally ‘Madee’ na kuongeza kuwa taarifa hizo ni za kuzusha.
Dogo Janja ameanika ubuyu huo siku chache baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa amenunuliwa gari na Madee.
Akizungumza na AMANI, mkali huyo kutoka Arusha, alisema hajawahi kununuliwa gari lolote, hivyo watu waache kuzusha mambo wasiyoyajua kwa kuwa gari zote huwa ananunua kwa pesa yake.
“Madee ni kweli anafanya biashara ya magari hilo nakubali, lakini sijawahi kununuliwa gari na Madee, huwa akileta gari kama nimelipenda, natoa pesa yangu mfukoni nanunua, kununuliwa gari na Madee ni kwamba sijiwezi sana au? Watu waache kuzusha mambo wasiyoyajua, mtu afanye uchunguzi kwanza ndipo waandike habari za kweli,” alisema.
No comments