Header Ads

Header ADS

Diamond Platnumz Aweka Rekodi Nyingine, Afikisha Views Bilioni 1 Youtube



Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya WCB Diamond Platnumz anazidi kufanya vizuri katika akaunti zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Youtube.


Kupitia akaunti yake ya Youtube Diamond ameweza kufikisha Views (Watazamaji) Bilioni Moja kutokana na maudhui mbalimbali anayoyaweka kupitia ukurasa wake huo.

Ikumbukwe Jarida kubwa na Billboard lilimtolea mfano kama msanii wa kuigwa na wasanii wa Kimagharibi namna ya kutumia akaunti ya Youtube kibishara, Billboard waliongeza kuwa Diamond ana uwezo wa kuweke zaidi ya video 20 kwa siku na katika akaunti yake hiyo akiwa na zaidi video 600.

Waliongeza kuwa katika wimbo mmoja Diamond ana uwezo wa kupandisha video tofauti tofauti ikiwemo Dance, Lyrics na video nyinginezo kupitia maudhui ya aina moja na katika huo wimbo mmoja ana uwezo wa kupandisha video 20.

Kwa namna hiyo huenda ndio kitu kilichochangia Diamond kufikisha Views bilioni moja katika akaunti yake ya Youtube.
Mbali na Diamond Billboard waliwatolea mfano wasanii wengine kama @burnaboygram @davidoofficial @wizkidayo @teknoofficial @nairamarley na wengine.

Hii inamaanisha Views (Watazamaji wote kwa ujumla kwenye akaunti yake waliowahi kutazama aidha ni video ya wimbo au show yoyote aliyowahi kuipandisha kwenye Youtube yake, hivyo watazamaji wote wakijumlishwa wamefika bilioni moja tangu aifungue hiyo akaunti Juni 12 mwaka 2011.

No comments

Powered by Blogger.