Chuki kati ya Nigeria na Afrika Kusini Inaendelea Kuwa ya Moto..Sho Madjozi na Burna Boy Waingia Katika Ugomvi Mkubwa
Hii ni baada ya Sho Madjozi kumtuhumu mwimbaji wa Nigeria Burna Boy kwa kufuta remix ya wimbo "Own It" wa Stormzy ambao mkali huyo wa Afrika Kusini ameshirikishwa, ikiwa ni mara baada tu ya wote kuwekwa kwenye kipengele kimoja (Best International Act) katika Tuzo za BET 2020.
Akiangusha mfululizo wa tweets, Sho Madjozi alisema kwamba Burna Boy alimuomba Stormzy kuushusha wimbo huo. SWIPE kuona tweets zake.
Mkali huyo mwimbaji wa Hit Song "John Cena" aliongeza kwamba walikuwa na mahusiano mazuri tu kabla ya kutajwa kwenye kipengele kimoja, alikazia kwamba Burna Boy aliomba ngoma hiyo ishushwe kwa sababu [Burna Boy] anamuhofia.
Akijibu mashambulizi hayo, Burna Boy aliweka wazi kwamba kuondolewa kwa wimbo huo kwenye mitandao ya muziki duniani hakuhusiani na yeye wala Tuzo, kwani Remix hiyo haikupitiwa vizuri na Label yake (Atlantic US)
"OWN IT sio wimbo wangu. Kama sauti yangu ipo kwenye wimbo huo kwa vyovyote inapaswa kupitiwa vizuri. Kama Remix hiyo haikupitiwa na label (Atlantic US) moja kwa moja wataichukulia hatua. Sihusiki kwa chochote wala masuala ya Tuzo." aliandika Burna Boy.
No comments