Header Ads

Header ADS

Beyonce Kutunukiwa tuzo ya Heshima Kwenye Tuzo za BET Mwaka huu.

Beyonce kutunukiwa tuzo ya heshima/ubinadamu kwenye Tuzo za BET mwaka huu.

Mwimbaji huyo amekuwa akitambulika kwa kazi yake kubwa, akifanya makubwa kupitia BeyGOOD Foundation, taasisi yake ambayo imefanya mengi tangu mwaka 2019 ikiwemo kusaidia kwenye elimu hasa kwa watoto wa Kike.

Pia ameshirikiana na UNICEF kutengeneza "BeyGood4Burundi" mradi ambao uliwekeza kuleta maji safi Afrika Mashariki. Aidha akishirikiana na Mama yake, Beyonce alianzisha (I Did My Part) mpango wa kuhamasisha wakazi wa Houston kupima virusi vya Corona na kuchangia vifaa na misaada mingine.

Tuzo za mwaka huu za BET zitahusisha pia mchango kwa Kobe Bryant toka kwa Lil Wayne na wengine. Zitarushwa moja kwa moja kupitia kituo cha BET, Juni 28 mwaka huu.

No comments

Powered by Blogger.