Baada ya 'Kiki' ya Kifo, Meja Aelezea Maisha yake
Mkali wa muziki wa singeli Meja Kunta, amenyoosha maelezo jinsi watu wanaomzunguka wanavyomchukulia kwa sasa, baada ya kujitengenezea kiki ya kifo mwanzoni mwa mwaka huu.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Meja Kunta amesema sasa hivi watu wanasapoti maisha yake na kila kitu anachokifanya kwa sababu, wamemuelewa na wameamua kumpokea tena.
"Watu wanasapoti sana maisha yangu na muziki wangu, wanatamani kuniona nafika sehemu fulani, wameamua kunipokea na Watanzania wamenielewa maisha mengine yanaendelea, pia watu wananipenda kutokana na ninachokifanya, wameamua kuishi kutokana na maisha yanavyoenda" ameeleza Meja Kunta.
No comments