Afrika Kusini Kuanza Majaribio ya Chanjo ya Corona
Afrika kusini imeanzisha majaribio ya kwanza ya chanjo ya virusi vya corona barani Afrika wiki hii, chuo kikuu kinachoongoza hatua hiyo kimesema leo, wakati nchi hiyo ikikabiliana na idadi ya juu ya kesi za maambukizi barani Afrika.
Chanjo, iliyotengenezwa na taasisi ya Oxford Jenner, tayari inafanyiwa tathmini nchini Uingereza, ambako washiriki 4,000 wametia saini kufanyiwa majaribio. Afrika kusini imepanga kuwapa chanjo watu 2,000 kwa kutumia chanjo hiyo inayofahamika kama ChAdOx1 nCoV-19.
Washiriki 50 katika ya wanaoshiriki majaribio hayo wana virusi vya HIV. Chuo kikuu cha Witwatersrand kimesema kuwa kilianza kuwateuwa washiriki kwa ajili ya majaribio ya chanjo hiyo ya Oxford 1 Covid-19 wiki iliyopita, na washiriki wa kwanza wanapata chanjo wiki hii.
No comments