Header Ads

Header ADS

Wadau Wadai MC Pili Pili Hapendwi na Mkewe Kuwa Alifuata Ustaa tu Kwake...MC Pili Pili Afunguka Mazito


Wadau Wadai MC Pili Pili Hapendwi na Mkewe Kuwa Alifuata Ustaa tu Kwake...MC Pili Pili Afunguka Mazito

KOMEDIANI wa Taifa ambaye pia ni MC matata Bongo, Emannuel Mathias ‘MC Pilipili’ amefungukia tetesi kuwa hapendwi na mkewe, Qute Mena kama ambavyo yeye anampenda.

Pilipili ameiambia Celebrity Bongo ya Gazeti la IJUMAA kuwa, watu wengi wamekuwa wakisema maneno hayo bila kujua ukweli ni upi, lakini anachokiamini yeye ni kwamba yeye na mkewe wanapendana kwa dhati na itakuwa hivyo hadi kifo kiwatenganishe.

“Kuna watu roho zinawauma mimi kumuoa huyu binti, ukweli ni kwamba najivunia mke wangu ni mzuri sana, tena kakamilika kila idara, ananipenda na mimi nampenda sana, hatujawahi hata kufikiria kuachana, sasa nashangaa kuona watu wanasema najipendekeza kwake,” amesema Pilipili.

Stori: Memorise Richard, Dar

No comments

Powered by Blogger.