Header Ads

Header ADS

Picha za Ngono zavuruga Vikao vya Bunge kwa Muda


Hili jambo lingetokea Bongo sijui ingewaje najaribu kuwaza tu kwakuwa mabunge mengi likiwemo la Tanzania hivi sasa linatumia teknolojia Zaidi katika kuendesha vikao vyake.

Imeelezwa kuwa huko Afrika kusini ambako wanendelea na lockdowan kufuatia janga la ugonjwa wa corona mkutano wa Bunge la nchi uliokuwa ukifanyika kwa njia ya mtandao umevurugika baada ya wadukuzi kutupia picha za utupu.

Asubuhi ya jana Mei 7, 2020 picha za ngono zilitokea katika skrini za wana mkutano huku sauti ya mwanamume ikisikika kumtusi Spika Thandi Modise, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.

South Africa Parliament Video Call Hacked With Pornography | TimeSpika huyo aliyeshikwa na hasira alipaza sauti akisema hiyo ndio sababu anapinga mikutano ya mitandaoni.

“Hiki kilichotokea ni kilekile nilichokuwa ninakisema kuhusu kufanya mikutano kwa njia ya ‘Zoom’ Modise amenukuliwa akisema hivyo na tovuti ya Times Live.

Wabunge walielezea tukio hilo kama lenye kukera na kutatiza akili, kulingana na Tovuti ya habari ya Eyewitness.

Hali hiyo Iliwalazimu wataalamu wa Bunge kutuma kiunganishi chengine ambapo wabunge waliunganika tena na kuendelea na kikao chao.

No comments

Powered by Blogger.