Header Ads

Header ADS

Mkuu Wa Mkoa Ataka Wabunge CHADEMA Wasaidiwe “Hawana Uhuru, Wanakatwa Mishahara”


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amewataka watanzania kuanza kuwatetea wabunge wa chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kutokana na kukosa furaha ndani ya chama chao

Hapi amesema kuwa wabunge wa CHADEMA wanakatwa mishahara yao kwa neno la mwenyekiti wa chama hicho  Freeman Mbowe bila ridhaa yao

“Wabunge wa Chadema huenda ndio wabunge wanaoongoza kutokuwa na furaha tangu vyama vingi vianzishwe nchini. Hawana uhuru na ubunge wao, wanakatwa mishahara yao ya ubunge na hawaruhusiwi kuwa na ndoto za uongozi isipokua kwa ruhusa ya “Mwenyekiti”. Tukemee huu udikteta uchwara.” Ameandika Hapi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter

Kauri ya Ally Hapi inakuja ikiwa ni siku hache Tangu kuzuka kwa mgongano kati ya bunge wa chama hicho juu ya kuhudhulia vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma


No comments

Powered by Blogger.