Geita: 5 Wafariki, 14 Wajeruhiwa Basi la Maiti Likigonga Lori
WATU watano wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya Coaster kuligonga lori la mizigo mkoani Geita. Imeelezwa kuwa basi hilo dogo lilikuwa likisafirisha mwili wa marehemu na waombolezaji kutoka Arusha kwenda Bukoba kwa mazishi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Loston, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema kuwa dereva wa lori alikuwa amepaki barabarani akiwa ametoka kwenda kutafuta vifaa ambavyo bado havijajulikana huku akiwa amechukua tahadhari ya kuweka matawi ya miti na reflectors kuashiria kuwa kuna gari imesimama.
Amesema kuwa dereva wa Coaster alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi na ndipo aliposhtukiza na kulivaa lori hilo kwa nyuma na kisha Coaster hiyo kuserereka na kwenda kusimama umbali wa mita mia. Amehitimisha kwa kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa Coaster.
No comments