Dawa ya Corona Yapelekwa NIMR Kuthibitishwa “Waliokuwa Hoi Wamepona, Tanzania Tunaweza Kuwa na Dawa Kama Madagascar”
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama amesema amefanikiwa kuwaibua Vijana waliotengeneza dawa inayokinga na kutibu corona ambayo tayari imepelekwa kwenye TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa ajili ya kufanyiwa utafiti, Mshama amesema pia Kibaha kuna dawa ya kujifukiza pamoja na viwanda vinavyotengeneza barakoa.
“Tumetengeneza barakoa na nimewaibua vijana wanatengeneza dawa hii (Bay Caro kiboko ya corona), kama una mafua, utaletewa dawa na anayekuletea na ataionja, unaweza kuletewa Watu wenye ushuhuda wakatoa ushuhuda walivyopona walipokuwa hoi na mafua makali”-DC Mshama
“Tunao uwezo wa kuwa na dawa kama Madagascar tusipodharau vya kwetu, tunayo pia dawa ya kujifukiza”- DC Mshama
No comments