Header Ads

Header ADS

Chura Anatafuta ‘Mchumba’ Nchini Bolivia


Wataalam wa kuhifadhi wanyama nchini Bolivia wameanza kutembea katika Taifa hilo zima wakimtafuta chura wa ‘kike’ atakayejamiana na chura mmoja asiye wa kawaida ambaye wanahofia kizazi chake huenda kikapotea kutokana na yeye kuwa peke yake.

Chura huyo aliyepewa jina la ‘Romeo’ mwenye umri wa miaka 10, anaishi katika maji na amekuwa akimtafuta mwenzake kwa kipindi cha miaka tisa. Tayari amewekwa katika mtandao wa kuwakutanisha wapendanao akisema ‘Namtafuta mpenzi juliet.’

Wanasayansi kwa sasa wanatafuta chura wa kike atakaye jamiana na Romeo katika madimbwi ya maji na mito ili kuhifadhi kizazi hicho.

Moja ya wanaomtunza amesema ”Hatutaki yeye apoteze matumaini. lakini wahifadhi hao watalazimika kuongeza kasi ya kumsaka chura huyo wa kike kwa kuwa hawezi kuishi zaidi ya miaka 15”.

Chura huyo anaishi katika pipa katika kumbukumbu ya Cochabamba amebakiza miaka mitano ya kuishi.

”Namtafuta Juliet wangu kwa sababu mimi ni kizazi cha mwisho cha familia yangu, Namtufuta chura wa kizazi changu, la sivyo kizazi changu chote kitaangamia”.

No comments

Powered by Blogger.