Agano la DAMU Katika Mahusiano ya Kimapenzi
Unapohusiana na mtu kimapenzi unafanya naye agano la damu. Agano hilo maana yake ni kwamba wewe unakubaliana na kufungamana na sifa na tabia pamoja na vifungo vingine vyote kama vile laana, mizimu, matatizo na majanga mbalimbali yanayomhusu huyo uliyefanya naye mapenzi, kadhalika na yeye anafungamana na wewe katika mambo hayo. Agano la namna hiyo humtaka aliyeingia katika hayo mapatano kukubaliana nayo "consistently". Iwapo mhusika hatatii au ataenda kinyume na agano, ndipo agano hilo "hutrigger malice" na kusababisha kutokuelewana, vurumai, kutokupendana na hata kuuana katika mahusiano na mara nyingi kupelekea kuachana!
Kimsingi, unapojamiana na mtu unakubaliana naye kuchangia kila kilicho chake, na yeye pia anakubaliana kuchangia na wewe kila kilicho chako, hasa laana na matatizo kama vile magonjwa na mizimu kwa sababu hivi vitu vimejengwa katika maagano ya damu.
Ndio maana wakati mnaoana na mwenzio mlipendana sana, lakini kwa sababu wewe au mwenzi wako alichepuka na kufanya maagano: ugomvi, mapigano, kutishiana, chuki na hata kutaka kuuana hakuishi kila leo! Swala sio wivu kwamba unahisi mwenzi wako anakusaliti au kuhitilafiana katika mambo tu ya kawaida, issue ni yale maagano ya damu ambayo "hudemand price"!
Mara nyingi unasikia watu wanalalamika kuhusu tabia za watoto "huyu mtoto tabia kaichukua wapi, mbona baba na mama yake au ukoo wao hawako hivyo?". Chanzo cha tabia za ajabuajabu za watoto ni matokeo ya michepuko iliyofanya maagano na watu/koo zingine zenye laana. Laana na matatizo yanayoletwa na agano la damu katika familia havihitaji mtu kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa, bali tu kuhusiana katika mapenzi!
Mimi nilipoingia kwenye mahusiano na mke wangu nilivunja maagano yote kwa jina la Yesu. Lakini kumbuka kuwa huwezi kuvunja maagano kama vile ya michepuko kwa jina la Yesu ili "kufavor your own evil deeds"!
Maagano yanayofanywa na watu kwa njia ya mapenzi huenda vizazi hadi vizazi. Hii ni sawa kabisa kwa mjibu wa sayansi kwani "hereditary information" kutoka kizazi hadi kizazi hubebwa na viasili vilivyopo katika damu, mfano DNA.
Pasco anaweza kuendeleza hii mada kwa uchambuzi zaidi.
Mie na mke wangu tuna furaha fulltime kwa sababu mapenzi yetu yananawiri kila kukicha, na huwa hatuelewi kabisa matatizo katika ndoa za watu yanatokana na nini! "We are the happiest couple" kwa sababu "we posses several life secrets" mojawapo ni siri kuhusu agano la damu!
Tambueni ya kwamba one of the great decisions a person can make in his/her life ni kuwa na uhusiano wa kimapenzi (hata kwa dakika moja) na mtu kwa sababu anafanya naye life covenant "blood covenant"!
We teach you things that matter most!
- LifeHacker
No comments