Wagonjwa Wa Corona Kenya Wafika 320....Ni Baada ya Wengine 17 Kuongezeka
Wizara ya Afya nchini Kenya imesema idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona sasa imefika 320 baada ya leo kutangaza visa vipya 17, vilivyotokana na sampuli 668 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.Kati ya hao, 12 ni kutoka miji ya Mombasa na 5 Nairobi.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Nchini Kenya Dkt. Mercy Mwangangi amesema wagonjwa 15 walichukuliwa na maafisa wa afya baada ya kuambatana na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa awali huku hao 2 wakiwa ndani ya karantini.
Wakati huo huo, Kenya pia imethibitisha kwamba wagonjwa 6 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona nchini humo kufikia 89.
No comments