Polisi waendelea kuchunguza sakata la wagonjwa wa corona kutoroka Amana
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la wagonjwa waliothibitika kuwa na virusi vya corona kudaiwa kutoroka katika Hospitali ya Rufani Amana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Camilius Wambura, aliliambia Nipashe jana kuwa, bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo baada ya juzi kupata taarifa za wagonjwa kutoroka hospitali hapo.
Juzi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alitoa ufafanuzi kuhusu taarifa za wagonjwa kudaiwa kutoroka Amana na kurejea nyumbani.
Mjema alisema kuna taarifa za wagonjwa hospitalini hapo za kulazimisha kuondoka ili kurejea nyumbani, lakini hakuthibitisha kuondoka kwao katika eneo hilo la matibabu.
No comments