Madaktari 251 Wapata Maambukizi ya Virusi vya Corona
Takriban madaktari 251 nchini Bangladesh wamepata maambukizi ya Corona Virus, Taasisi ya Madaktari (BDF) imelalamikia ukosefu wa vifaa kinga (PPE) kuwa chanzo cha Madaktari kupata maambukizi kutoka kwa wagonjwa
Kufuatia ongezeko la waathirika wa COVID 19 nchini humo, Serikali imekuwa na changamoto ya kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi ya Virusi hivyo.
Bangladesh, kama ilivyo kwa mataifa mengi duniani inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa kinga kwa ajili ya watoa huduma za afya. Nchi hiyo imerekodi maambukizi 4,186 na vifo 127 hadi sasa huku waliopona wakiwa 108.
No comments