Header Ads

Header ADS

Lema akubaliana na Rais Magufuli Taifa liombewe kwa siku 3, achomekea na mengine


Mbunge wa Chadema Godbless Lema amewataka watu kuungana na Rais John Magufuli katika kuliombea Taifa kwa siku tatu ili atuepushe na madhara ya ugonjwa wa virusi vya Corona (Covid-19).

Lema amesema hayo Muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwaomba Watanzania kila mmoja kwa kuanzia kesho kuliombea taifa kwa siku tatu mfululizo. Lema amesema hiyo ni hatua nzuri inayoleta matumaini huku akisema yeye na familia watafanya hivyo.
“Rais Magufuli ameomba tumuombe Mungu kwa siku 3 ili atuepushe na madhara ya Covid 19,ni hatua nzuri kujua uwezo wa Mungu,inaleta matumaini kwa siku za baadae,kwani SALA/UPENDO ni ndugu.Mimi/Familia yangu tutaomba.Arusha/Tanzania tuungane na Rais ktk Sala huku tukiendelea kujikinga”


No comments

Powered by Blogger.