Header Ads

Header ADS

Hivi ndivyo Mazishi ya Mama Rwakatare yalivyokuwa


Tayari mwili wa Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mikocheni B, Assemblies of God, Askofu Dkt Getrude Rwakatare, umekwishapumzishwa katika nyumba yake ya milele, katika viunga vya kanisa hilo, jijini Dar es Salaam.


Mazishi hayo yamefanyika Alhamisi ya leo ya Aprili 23, 2020, majira ya saa 7:00 mchana na kuhudhuriwa na watu kadhaa ndani ya familia.

 Baadhi ya watu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Askofu Dkt Getrude Rwakatare.

Mama Rwakatare alifariki Dunia Aprili 20, 2020, katika hospitali ya Rabininsia, alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo kwa mujibu wa mwanaye Mutta Rwakatare, alisema kuwa Mama yao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na presha.


Kaburi la Mama Rwakatare, likiombewa.

Mungu ailaze Roho ya marehemu, Mama Getrude Rwakatare, mahala pema. Amina.



No comments

Powered by Blogger.