Everton Yamuwinda Mbwana Samatta
Baba mzazi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta amefunguka kuwa anaamini mtoto wake ataendelea kucheza Ligi Kuu England hata ikitokea Aston Villa ikishuka daraja kwa kuwa tayari timu ya Everton imejipanga kumchukua.
Mshambuliaji huyo amejiunga na Villa kwa mkataba wa miaka minne na nusu katika kipindi cha dirisha dogo akitokea KRC Genk ya nchini Ubelgiji.
Mzee Samatta amesema kuwa kwa sasa mtoto wake anaendelea kufanya mazoezi binafsi kwa lengo la kutaka kuisaidia timu yake isishuke daraja lakini hata kama itatokea kushuka basi atajiunga na Everton kwa kuwa wameonyesha nia ya kutaka kumnunua ikiwa Aston Villa watashuka daraja.
“Samatta amekuwa akifanya mazoezi binafsi kwa sababu ya Corona na ukiangalia hata familia yake ipo kule baada ya kwenda kumtembelea, anachokiangalia kikubwa ni kuona Villa wanabaki katika Ligi Kuu England na wapo kwenye nafasi mbaya.
“Suala la kushuka thamani siyo ishu sana kwa sababu Everton wamekuwa kwenye mawindo ya kuweza kumnunua kama itatokea Villa wanashuka daraja,” alisema mzee Samatta.
No comments