"Waliniambia Maini yameoza Lakini Haikuwa Kweli"-Hawa Ntarejea Afunguka
EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na Hawa Ntarejea, ambaye amesema kipindi anaumwa alikuwa anasikia maneno mengi kutoka kwa watu ambao anahisi, walikuwa wanatamani afe.
Msanii huyo wa BongoFleva amesema matatizo yaliyomtokea alijitakia mwenyewe na chanzo ilikuwa ni pombe, ambapo aliambiwa maini yake yameoza na tumbo limejaa kumbe sio kweli, shida Iliyokuwepo ni moyo na mishipa kushindwa kufanya kazi.
"Neno pombe limenifanyia kitu kibaya sana kwenye maisha yangu, japo sasa hivi nipo sawa na naweza nikanywa ila tangu yaliyonitokea sitamani tena, tumbo langu lilijaa wakasema maini yameoza lakini sio kweli, tatizo lilikuwa ni moyo na mishipa ilikuwa haifanyi kazi vizuri ndiyo maana nikawa najaa maji tumboni" ameeleza Hawa Ntarejea.
Aidha ameendelea kusema
"Maini na bandama vyote vipo salama, hata pombe naweza nikanywa tena, nimeonekana naumwa na nimepata kashfa nyingi kwa sababu ya pombe na kipindi cha ugonjwa unavumilia tu, lakini mengine ukisikia unasema hawa watu wanatamani mimi nife nini" ameongeza.
No comments