Ushauri: Mume Hataki Kufanya Mapenzi na Mimi, Anamtaka Mtoto Niliyezaa Kabla ya Kunioa
Naombeni ushauri wenu,
Mawazo ya wengi ndio nitakayoyafanyia kazi. Nimefunga ndoa na mwanaume mwenye watoto 4 wawili wakike wawali wa kiume. Mama yao alifariki kwa ajali ya gari aliwaacha wadogo wakiwa primary.
Na mimi niliolewa nikiwa na mtoto mmoja wa kike ambae kiumri analongana na mtoto wake watatu. Kusema ukweli mwanzoni iliniwia ngumu sana kukubali ombi lake hasa nikifikiria kulea watoto wa mama mwingine wanikubali, je, vipi kuhusu huyu nilienae?
Baada ya muda kupita na kukolea kimapenzi nilijubaliana nae tukafunga ndoa tukaunganisha familia wote wakawa kitu kimoja. Mungu akabariki tujaliwa kupata mtoto mmoja. Kiukweli niliwapenda sana hawa watoto, niliwalea kama wangu.
Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwafanya wasijione wakiwa. Kama zawadi nk nilitowa mezani bila kubagua sikupenda kuweka makundi na hili shahidi ni Mungu pekee. Watoto watatu wapo chuo kikuu na mmoja wa kwake yupo form six.
Katika ndoa yangu kulikua na migongano upande wa tendo la ndoa, kabla ya ndoa tukiwa kwenye stori za mapenzi niliwahi kumweleza mwenzangu kuwa mimi sio mtundu sana upande wa sex ivyo ningependa yeye awe mwalimu kwangu kwani tangu mwanaume wa kwanza anidanganye na kunipa ujauzito sikuwa tena kuwa na byfriend.
Akiniambia sawa. Tulipoingia kwenye ndoa mwenzangu alianza kubadilika wakati mwingine alikaa hata miez 8-10 bila kutaka sex.Nikimuuliza husema amechoka au hajisikii.
Hata huo muda anaokaa mpaka mimi nimchokoze na hii nikutakana na kushindwa kuvumilia. Kuna wakat aliamua kuniambia ukweli kuwa sijui mapenzi, niliumia ila nilikubali kuwa ni kweli sijui ila anisaidie kujua.
Hakufanya ivo. Ilifikiwa wakati nikaona ngoja nikae nisimsumbue ila nilijiuliza nitaishi hivi mpaka lini na kusaliti ndoa siwezi. Nilimwomba Mungu sana anipe uvumilivu ila pia Mungu aseme na mimi juu ya hii ndoa.
Mungu ni mwaminifu. Baada baada ya maombi ya zaidi ya mwaka mke wa shemeji yangu alileta malalamiko kuwa mume wangu amekua akimsubua sana kimapenzi ikiwa ni pamoja nakumtumia picha za ex.
Niliziona hakuishia hapo akasema hata hawa wadada wa kazi huwa anatembea nao. Nilipowabana waliopo na walioondoka walikubali na kunipa ushahidi. Mbaya zaidi hata huyu mwanangu alishamtaka kimapenzi sina uhakika kama alifanikiwa au la.
Ninaumia sana sana. Mtaani ndoa yangu imekua mfano wa kuigwa hio ni kutokana na jinsi tunavoonekana kwa watu. Lakini hii yote onatokana na jinsi nisivopenda watu wajue mambo ya ndani. Ninampenda, ninamheshim, ninamjali.Siruhusu nguo au chakula cha mume wangu afanye mwingine nikiwepo.
Hata kama tumegombana nisingependa yoyote ajue, nilijitahidi sana, kuwa mtiifu na mnyenyekevu kwake. Hii nikutokana na malezi niliyolelewa. Hata kama amesafiri watoto watajua baba anarudi kwakua wataniona jinsi ninavokua busy jikoni na kuandaa juisi na matunda.
Ushauri wenu muhimu sana kwangu
Asanteni
No comments