Rais Xi Jinping atembelea Wuhan mji ulioathirika zaidi na Corona
Rais wa China Xi Jinping ameutembelea mji wa Wuhan leo kwa mara ya kwanza tangu mji huo ulipokumbwa na janga la mlipuko wa virusi vya Corona mnamo mwezi Januari.
Ziara ya Xi imekuja baada ya hatua ya mji wa Wuhan na mkoa wa Hubei kuwekwa kwenye Karantini tangu mwishoni mwa mwezi Januari kuonesha kufanikiwa ambapo maambukizi mapya yamepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindio cha wiki za karibuni.
Hata hivyo hatua ya Rais kutembelea Wuhan ambako ni kitovu cha maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona nchini humo ni dalili kubwa inayowafanya maaafisa kuamini kuwa mripuko huo umethibitiwa
Hatua iliyopigwa China ni kinyume na jinsi mgogoro huo unavyoendelea kutanuka duniani ambapo sasa unasambaa kwa kasi kubwa nje ya China na Itali imeanza kutekeleza hatua ya Karantini nchi nzima
No comments