Header Ads

Header ADS

Nandy Yamkuta Makubwa YOUTUBE "Naona Miujiza tu Kwenye Account Yangu Naombeni Mnisaidie"




Msanii wa kike anayefanya vizuri hapa nchini Nandy, ameeleza kuwa zimepita siku nne sasa ambazo anajionea miujiza katika mtandao wa Youtube, ambapo anahisi kuna mchezo mbaya anafanyiwa na baadhi ya watu baada ya idadi ya watazamaji wa video yake kupungua.


Akitoa taarifa hiyo kupitia post aliyoweka katika mtandao wa Instagram, Nandy amesema anafanyiwa vitu vya ajabu sana, watu wanamrudisha nyuma kwani idadi ya watazamaji katika video ya wimbo wake wa na nusu wanapungua.

"Nimevumilia hii siku ya nne sasa, huko Youtube kunatokea vitu vya ajabu sana sijui nini tatizo, ikifikisha watazamaji laki tisa, wanarudishwa nyuma hadi laki nane au saba, naona miujiza tu kwenye akaunti yangu, sitaki kuhukumu watu naomba watu wa ufundi wanisaidie kujua kuna nini" ameandika Nandy.


No comments

Powered by Blogger.