Mtanzania wa Kwanza Ugundulika Kuwa na Virusi vya Corona
Abu Dhabi: Wizara ya Afya ya Falme za kiarabu (U.A.E) imethibitisha kwamba Raia mmoja wa Tanzania ni miongoni mwa Watu 15 wapya waliokutwa na virusi vya corona.
Watu hao 15 wenye maambukizi mapya ni Mtanzania mmoja, mmoja wa South Africa, mmoja Iran, Mjerumani mmoja, Waitalia watatu, wawili wa U.A.E, Wasrilanka wawili, Waingereza wawili na wawili wa India.
Tayari wameshawekwa chini ya uangalizi maalum na wanaendelea vizuri ambapo inaeipotiwa baadhi yao waliambukizwa na Wagonjwa wengine waliotoka nje ya Nchi na hakuna taarifa zaidi yakiwemo majina yao.
Mpaka leo March 10 kuna Wagonjwa wa corona zaidi ya laki moja na elfu 14 duniani, vifo zaidi ya 4000 na sasa Shirika la Afya linasema idadi ya wanaopona inazidi 70%.
No comments