Header Ads

Header ADS

Mkude: Tukiwafunga Tu Yanga, Sisi Mabingwa



KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, ametoa kauli ya kuikatisha tamaa Yanga baada ya kusema kwamba, timu yao leo ikifanikiwa kuibuka na ushindi, basi watajihakikishia ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Timu hizo mbili zitachuana leo Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo mechi ya mzunguko wa kwanza ilimalizika kwa sare ya 2-2.
“Tumejipanga vilivyo kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo dhidi ya Yanga kwa njia yoyote ile. “Ushindi huo ni muhimu sana kwetu kwani utatufanya tuwe katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya tatu mfululizo.
“Binafsi kama tutashinda mchezo huu tunaweza kujitangazia ubingwa wa ligi kuu kwani hatutakuwa na timu nyingine tishio inayoweze kusababisha tusitimize ndoto zetu hizo,” alisema Mkude. Kwa sasa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 26, Yanga inazo 47 katika mechi 24.


No comments

Powered by Blogger.