Kwa Tshishimbi, Hapa Wamelamba Dume
KIUNGO Papy Kabamba Tshishimbi ni jembe kweli na ukiwa naye kikosini kwako, basi umelamba dume.
Kwa takribani wiki nzima, kulikuwa na tetesi kwamba kiungo huyo wa Yanga anataka kuhamia Simba, huku akiwa bado hajakubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga.
Tetesi hizo zimevuma sana huku mwenyewe akikiri wazi kwamba yupo tayari kuitumikia timu ambayo itakuwa na maslahi mazuri kwake.
Sasa unajua ni kwa nini, hivi sasa Tshishimbi amegeuka kuwa lulu na kugombewa sana, ni kwa sababu ya kiwango alichokionyesha msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.
Mkongomani huyo anayevaa jezi namba 24 huku kichwani akiwa amefuga rasta, kwa msimu huu hadi sasa amewakimbiza wachezaji wa kigeni wanaokipiga ndani ya Simba wanaocheza nafasi ya kiungo.
Yanga ikiwa imecheza mechi 27 za ligi kuu msimu huu, Tshishimbi amecheza mechi 23 na kutumika kwa dakika 1936 ambazo ni nyingi kuliko zilizotumiwa na viungo wa Simba.
Kwa upande wa Simba, kiungo aliyetumia dakika nyingi uwanjani ni Clatous Chama ambaye amecheza mechi 23 kati ya 28 na ametumia dakika 1745 akifuatiwa na Francis Kahata ambaye amecheza mechi 22 kwa dakika 1452. Sharaf Shiboub amecheza mechi 20 kwa dakika 1051, huku Deo Kanda akicheza mechi 14 kwa dakika 590.
Mechi ambazo Tshishimbi amecheza ni dhidi ya Ruvu Shooting (dk 90), Mbao (dk 90), JKT Tanzania (dk 90), Mbeya City (dk 90), KMC (dk 90), Prisons (dk 26), Biashara United (dk 20), Ndanda (dk 90), Alliance (dk 90), Simba (dk 90), Azam (dk 90), Singida United (dk 90), Mtibwa Sugar (dk 90), Lipuli (dk 90), Ruvu Shooting (dk 90), Mbeya City (dk 90), Prisons (dk 90), Polisi Tanzania (dk 90). Coastal Union (dk 90), Mbao (dk 90), Simba (dk 90), KMC (dk 90) na Namungo (dk 90).
No comments