Kamanda wa Al-Shabab Bashir Mohamed Qorgab 'auawa katika shambulio la angani '
Shambulio la angani nchini somalia limemuua kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la al-Shabab, tripoti zinaarifu nchini humo .
Marekani ilitoa zawadi ya dola milioni tano sawa na (£3,8m) mwaka 2008 kwa yeyote atakayewasilisha taarifa kuhusu alipo Bashir Mohamed Qorgab.
Marekani imekuwa ikifanya mashambulio ya angani ya mara kwa mara nchini Somalia ikiwalenga wanamgambo wa al-shabab.
Alikuwa kiongozi wa mashambulio dhidi ya kambi za kijeshi, na alihusika na oparesheni ya kundi hilo nchini Kenya, ilisema ripoti hiyo.
Qorgab aliuawa Februari 22 Februari katika mji wa Sakow kusini mwa Somalia, katika oparesheni ya pamoja kati ya majeshi ya Somalia na Marekani, Kito ya radio cha nchi hiyo iliripoti, Lakini haikufafanua kwanini taarifa hiyo inaangaziwa wakati huu.
Mwezi uliopita taarifa ambazo hazikuthibitishwa katika vyombo vya habari vya Somali ziliripoti kuwa Qorgab ametengana na Al-Shabab baada ya kutofautiana na viongozi wengine.
Kundi la Al-Shabab linalohusishwa na al-Qaeda linathibiti maeneo ya kusini na kati ya Somalia.
Kundi hilo ambalo limefanya msururu ya mashambulio ya mabomu katika nchi jirani ya Kenya, linasadikiwa kuwa hatari zaidi katika eneo hilo.
Mwezi uliopita, wapiganaji wa kundi hilo walishambulia kambi ya kijeshi inayotumiwa na vikosi vya Kenya na Marekani, na kuwaua wanajeshi watatu- mfanyikazi mmoja wa jeshi la Marekani na wajenzi wawili.
No comments