Iran: Maambukizi ya Corona yaongezeka
Iran jana imeripoti visa vipya zaidi ya 1,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya siku moja huku idadi ya vifo ikipanda na kufkia watu 145 katika Jamhuri hiyo.
Msemaji wa wizara ya afya nchini humo amesema kuwa jumla ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo imefikia watu 5,823 na maafisa kadhaa wa serikali ni miongoni mwa watu waliokufa kutokana na Corona.
Jana vyombo vya habari nchini Iran vililiripoti kuwa mbunge aliyechaguliwa hivi karibuni Fatemeh Rabar alifariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Maafisa 12 wa serikali, akiwemo makamu wa rais anayeshughulikia masuala ya wanawake na familia Masoumeh Ebtekar wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo. Mamlaka za nchi hiyo zimesema maambukizi yamesambaa zaidi kwenye mji mkuu, Tehran.
No comments