Header Ads

Header ADS

Breaking News: Hukumu ya Mbowe, Wenzake Yaahirishwa kwa Muda




HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, ameahirisha kusoma hukumu ya kesi inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hadi saa 7:30 mchana ambapo tayari watu mbalimbali wamehudhuria kwenye usomwaji wa hukumu hiyo akiwemo Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif.

Mahakama hiyo ilitarajiwa leo Machi 10, 2020, kutoa hukumu ya kesi inayowakabili viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wake aliyehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Vincent Mashinji.

“Nimefika Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu, Dar es Salaam kusikiliza hukumu dhidi ya viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe ikiwa kuonyesha mshikamano wangu na wa chama cha ACT – Wazalendo katika yale wanayopitia. Pamoja Daima,” amesema Maalim Seif.



No comments

Powered by Blogger.