Sababu yatajwa wanaume wengi kukosa nguvu za kiume
Serikali imetaja sababu ya wanaume wengi kukosa nguvu za kiume.
Ambapo ugonjwa wa Kisukari pamoja na msongo wa mawazo vimetajwa kuwa ndiyo visababishi vikubwa kwa mwanaume kukosa nguvu za kiume.
Tatizo la wanaume wengi kukosa nguvu za kiume limekithiri sana na Serikali inatambua uwepo wa dawa za kuongeza nguvu za kiume dawa zisizo na kemikali ambazo hazijatangazwa rasmi.
Hayo yameelezwa jana Bungeni na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Dk Hussein Mwinyi aliyekuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alihehoji sababu ya wimbi kubwa la wanaume kukosa nguvu za kiume na kupelekea uwepo na uhitaji mkubwa wa dawa hizo.
Waziri Mwinyi ambaye alijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa kuna sababu nyingi zinazochangia kupungukiwa na nguvu za kiume.
Aidha, Serikali inatambua uwepo wa dawa kwa ajili ya wanaume ambazo hazina kemikali na ameonya matumizi ya dawa ambazo hazijafanyiwa utafiti kwa kuwa si salama kwa ajili ya matumizi.
No comments