Rais Magufuli awapa dole gumba wakazi wa Kyela, Amtumia salamu Mwakyembe ‘natamani siku niwe waziri wa michezo
Rais Magufuli yupo mkoani Mbeya kwenye ziara yake ya kikazi ya siku 8, ambapo leo Aprili 30, 2019 ametembelea katika wilaya za Tukuyu na Kyela.
Akiwa Wilayani Kyela, Rais Magufuli amewapongeza wakazi wa Kyela kwa kluchagua Mbunge na madiwani wengi wa CCM, huku akioneshwa kuumizwa na matokeo ya timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys ambayo ilipoteza michezo yote mitatu kwenye michuano ya Afcon U-17 .
Rais Magufuli amesema kuwa angetamani siku moja kuwa Waziri wa Michezo kwani angekisuka kikosi hicho yeye mwenyewe, ili kipate matokeo kwani ameshangazwa na timu zetu za taifa kufungwa hovyo hovyo, licha ya kuwa Tanzania ni Taifa lenye watu wengi kuliko hata hizo nchi zinazowafunga.
No comments